Kulingana na taarifa zilizotolewa na mtandao wa habari wa
Nigeria Dailytimes.com, chanzo chake kimeeleza kama ifuatavyo.
“Ndio
wamegombana wiki hii. Kiasi cha kufikia Peter kumchokoa kwenye jicho la kushoto Paul
kwa kidole. Lakini mgogoro huo haukutokea wakati wa mazoezi kama
inavyosemekana, bali Peter amegoma kufanya jambo lolote la P-Squar kwa muda wa
wiki nzima.
Walialikwa kuburudisha kwenye harusi moja ya Raisi Jonathan
lakini hawakutokea. Peter alitoka nje na kusema kuwa Paul na kaka
Jude wanamtenga. Anasema kuwa wanafanya hivyo kwasababu katika nyimbo 2000,
1999 zilikuwa ni nyimbo ambazo zimefanywa na Paul. Kutokana na hali hiyo, ndugu
zake hawo wanamuita Mnenguaji katika kundi hilo la P-Square. Peter amekasirishwa sana na kauli hiyo.
Pia peter akashusha lawama kwa
kaka yake Jude kuwa hamheshimu mke wake. Jambo ambalo limepelekea Peter na Jude
kuto kuzungumza kwa takribani wiki nzima. Peter anasema kuwa Jude hana heshima
kwa mke wake kwa miaka mingi sana. Pamoja na kwamba Lola mke wa Peter ni mkubwa
kwa Jude lakini bado haoneshi heshima. Kama utakumbuka Jude hakuhudhuria kwenye
harusi ya Peter mwaka jana ingawa alikuwepo Nigeria.
Ndugu wa familia hiyo wanasema
kuwa Peter alilazimishwa na mwanamke huyo kumuoa lakini hayakuwa makubaliano
yao. Kwa maana hiyo katika familia nzima hakuna hata mtu mmoja ambaye
anamkubali mke wa Peter.
Mtafaruku huwo umekuwa kiasi cha
kufikia hatua ya kumuita mwanasheria kwaajili ya kugawana vitu ambavyo walikuwa
wanavimiliki kwa pamoja. Jude amesema kuwa amejitahidi kwa kadri ya uwezo wake
kuona utofauti huwo unafutika lakini ameambulia patupu.
Mashabiki wanawaomba sana
wanamuziki hao wamalize tofauti zao na kurudi kazini kwa pamoja. Mashabiki wa
P-Square wanaonekana kujawa na hofu kwa kuharibika kwa muziki wa wanandugu hao
hasa kama hawatakuwa pamoja katika kazi zao.