Katika hali ya kusikitisha mwanamke mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuingiliwa kimwili kwa nguvu na wanaume watano akiwemo askari wa jeshi la polisi.


Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii ni kwamba, mwanamke huyo amejikuta katika sakata hilo pale alipokuwa amekwenda kumtembelea rafiki yake wa kiume kwa lengo la kufanya naye mazungumzo.
Alipofika nyumbani kwa rafiki yake huyo baada ya muda walifika wanaume wanne akiwemo rafiki yake na kumfunga kamba kisha kumuingilia kwa zamu akianza na yule rafiki yake.

Kutokana na vitisho alivyokuwa akipewa mwanamke huyo ilimbidi avumilie hadi wanaume wote hao walipomaliza na kumuachia huru.

Chanzo cha habari kimeendelea kufunguka kuwa, baada ya kutoka pale mwanamke huyo alikwenda moja kwa moja hadi kituo cha polisi kwa lengo la kushitaki. Alitoka na askari ambaye jina lake limehifadhiwa hadi nyumbani kwa rafiki wa mwanamke ambaye amefanyiwa vitendo vile vya kinyama, lakini kwa bahati mbaya watuhumiwa hawakuwepo.

Askari alimchukua mwanamke yule na kwenda naye nyumbani kwake kwa lengo la kutaka kumpeleka hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu, lakini alimgeukia mwanamke huyo na kumlazimisha kufanya naye mapenzi. mwanamke alipokataa ndipo askari huyo alipoamua kumuingilia kwa lazima na kuongeza idadi ya wanaume waliombaka mwanamke huyo kufikia watano.

Askaria aliyehusika na tukio hilo alifikishwa mahakamani na kusomewa shitaka lake mjini Abuja, Nigeria. kisha alihukumiwa miaka saba jela kwa kosa hilo la ubakaji.

Bofya hapa kujiunga na Ukurasa wetu wa Facebook tukuhabarishe kila siku>>

 
Top