Maafisa watendaji wa vijiji wameonekana kuhusika kwa namna moja ama nyingine katika vitendo vya ukatili vinavyoendelea mkoani Mbeya.


Hali hiyo imejidhihiisha baada ya wawezeshaji wa mradi wa GBV unaojihusisha na masuala ya ukatili wa Mwanamke kutishiwa maisha yao wanapotoa taarifa kwa maofisa wa serikali ambao hawachukui hatua yoyote dhidi ya wahalifu.

Jambo ambalo linalalamikiwa na wawezeshaji hao ni kwamba pale taarifa zinapopelekwa ka viongozi hao wa kijiji, kinachotokea ni kwamba viongozi huwaita wahalifu na kuwatajia watu ambao wamepeleaka taarifa hizo serikalini.

"Watendaji wanahusika mojakwamoja katika matendo ya ukatili kwasababu mtu anapopeleka taarifa za ukatili hawachukui hatua zozote na badala yake huwataja watoa taarifa kwa mlalamikiwa" alisema muwezeshaji mmoja.

Watendaji hawafanyi kazi kama kazi inavyotaka bali wanafanya kazi kama wako nyumbani. Hivyo wanahofia kuonekana tofauti katika jamii kwa kuwachukulia hatua watu wa nyumbani.
 
Top