Watu wawili wanaodawa kuwa ni wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu mkoani Dar es salaam jana kujibu shitaka.
Watu hao wamefikishwa mahakamani hapo baada ya tukio lililotokea juzi Makaomakuu ya polisi walipokuwa wakipambana na polisi baada ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuitwa na jeshi la polisi kutoa maelezo kufuatia kauli yake liyoitoa siku kadhaa zilizopita inayochochochea maandamano ya nchi nzima.
Wakati watu hao wakifikishwa mahakamani kujibu shitaka hilo, mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe ameripotiwa kusafiri kuelekea Afrika Kusini. Utamu wa Raha haikuweza kubaini kiongozi huyo amekwenda Afrika Kusini kufanya shughuli gani.