Kamanda a Polisi Mkoani Kagera
Henery Mwaibambe ameeleza waandishi wa habari muda mfupi uliopita kuwa, askari
hao na mwenzao aliyewapiga picha wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi.
Kwa Mujibu wa chanzo cha Habari hii kimeeleza kuwa, kitendo hicho kimefanywa na askari hao mwaka 2012, ambapo walipiga picha hizo wakiwa kazini kisha kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kazi yao.
Amesema kuwa PC Fadhili ndiye aliyekuwa akifanya shughuloi hiyo ya kuwatwanga wenzake picha kwa kutumia simu yake ya kiganjani kisha kuzisambaza katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Kamanda Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788, PC Fadhiri Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme, wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Misenyi, mkoani Kagera.
Aidha Mwaibambe ameeleza kuwa Picha zinazoonekana ni halisi na hazija chakachuliwa. Hivyo kila skari polisi aweze kutambua kuwa jeshi lina maadili yake ambayo wanapaswa kuyafuata.