SEHEMU YA KWANZA:
Ilikuwa nii majira ya saa sita za mchana katika kijiji cha M'bete kilichopo kwenye milima ya uruguru iliyosimama kando kidogo ya mji mdogo wa Morogoro. Miguu ilikuwa ikituwaka moto kutokana na kupandisha milima hiyo, hasa mimi ambaye nilikuwa mgeni wa mazingira.

Nilikuwa nikivuta hatua kiuchovu nyuma ya msichana mrembo wa Kiruguru aliyekuwa akifahamika kwa jina la Kibena. Ninaposema mrembo ninamaanisha ni mrembo kweli. Binti yule ambaye hakuwa mrefu wala hakuwa mfupi alijaaliwa maumbile yenye kuvutia na yasiyo chosha macho ya mwanamume yeyote hata asiye rijali kumkodolea macho. Chini ya kiuno chake kwa nyuma alikuwa na kafurushi kalikokuwa kakivutia kutokana na ufundi wa Muumba. Kila tulipotembea macho yangu hayakuchoka kukakodolea kafurushi kale ambako hakakuwa kakubwa sana lakini kalikokuwa kanavutia.  Msichana yule mrembo alikuwa na ngozi laini yenye rangi nyeusi iliyokuwa na weupe kwa mbali lakini haikuwa rangi ya maji ya kunde.
Ingawa sauti ya mziki wa redio ambayo nilikuwa nimeikamatia kwenye mkono wangu wa kulia ilikuwa ikijitahidi kunibembeleza na kuniliwaza kila nilipokuwa nikipandisha mlima lakini nilihisi nguvu zikiniishia. Nilisimama na kushika kiuno huku macho yangu yakiwa kwenye miguu ya Kibena ambayo ilikuwa imekomaa ingawa haikuwa myembamba ya kuchukiza. Kibena alipohisi nimesimama akageuka na kunitazama.
“Vipi mpenzi?”
“Hatufiki?” Niliuliza kwa sauti iliyoonesha kukata tamaa. Kibena akanisogelea na kunishika mkono.
“Bado kidogo mpenzi jitahidi” Kibena lizungumza huku akinivuta kidogo mkono
wangu.
 “Kwanini mnaishi mbali hivi Kibena”
“Mie ndio nimezaliwa huku huku. Tunakwenda palee kwenye ile nyumba nyeupe”
Kibena aliniambia huku akinionesha nyumba moja iliyokuwa juu sana kwenye mlima ule tulio kuwa tukiukwea. Nilipopaona pale aliponionesha nikajikuta nikitoa pumzi kwanguvu.
“Kule ndiko unasema bado kidogo?” Niliuliza kwa mshangao.
“Jikaze bwana. Inamaana utakuwa huji kuwasalimu wakwezo?”
“Mnh! haya bwana, ukipenda boga penda na ua lake” Nilizungumza na kuanza kuvuta hatua kupandisha mlima ule.
“Habari ndiyo hiyo baba” Kibena aliniambia kisha sote tukaangua kicheko. Jamani nyie acheni tu. Nilijichekesha kinafki tu lakini nilitamani kugeuza na kurudi.
Tulipo fika karibu na pale aliponionesha Kibena tulisikia sauti ya ngoma. Sikuona sababu ya kuvumilia ikabidi niulize.
“Hiyo ni ngoma ya nini Kibena?”
“Huo ni mdundiko. Ngoma yetu ya asili”
“Kwahiyo inapigwa kwa madhumuni gani?” Niliuliza kwasababu kwenye mila ya kwetu ya Kinyakyusa kila ngoma inapigwa kwa madhumuni maalumu.
“Huwa mara nyingi inapigwa kwenye sherehe mbali mbali kama vile za harusi ama sherehe za unyago” Kibena alifafanua.
“Lakini pale si ndipo uliponionesha na kusema kuwa ni nyumbani kwenu?”
“Ni kweli hata mimi nashindwa kuelewa, sijajua kinacho endelea. Twende tutajua huko huko.”
Itaendelea......

 __________________________________________________________________








 
Top