Waokoaji wakiendelea na juhudi zao eneo la tukio
Watu 8 wameripotiwa kufa na wengine zaidi ya 20 hawajulikani walipo baada ya boti ya MV VIPE kuzama katika ziwa Tanganyika.
KIGOMA:Kwa mujibu wa chanzo cha Habari hii kimeeleza kuwa, Boti hiyo iliyokuwa ikiunganisha Tanzania na Kenya Imezama leo mchana ilipokuwa karibu na fukwe za mjini Kigoma katika kijiji cha Kalalangabo wilayani Kigoma.
Msemaji wa Polisi Advera Senso amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa boti hiyo iliyokuwa imebeba jumla ya watu 90 ilizama katika ziwa Tanganyika.
Alisema kuwa boti hiyo ilizama baada ya kugonga mwamba katika ziwa Tanganyika kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma na kuifanya iyumbe.
Alisema kuwa boti hiyo ilizama baada ya kugonga mwamba katika ziwa Tanganyika kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma na kuifanya iyumbe.
"Ulitokea upepo mkali na kusababisha boti kuzama. Na hadi sasa miili ya watu 8 imepatikana na wengine zaidi ya 20 hawajulikani walipo" alisema na kuongeza kuwa watu 60 waliweza kuokolewa wakiwa hai.
INNALILAHI WAINA ILLAIHI RAJIUN, BWANA ALITOA BWANA AMETWAA - JINA LAKE LIHIMIDIWE.... EMEN
Chanzo AFP