Kisu kikiwa kimeingia kwenye tumbo la mwanafunzi Moza
KWA UFUPI:
ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza ambaye aliamua kujididimiza kisu tumboni kwake akiamini ndio suluhu la tatizo lake.

HABARI KAMILI:
IRINGA: Mwanafunzi mmoja wa chuo cha Uhasibu TIA huko mkoani Iringa aliyefahamika kwa jina la Moza amenusurika kufariki dunia baada ya kujichoma kwa kisu tumboni jana.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii Kimeeleza kuwa; Moza ameamua kuchukua maamuzi hayo ya kutaka kujitoa uhai wake, baada ya kumfumania mpenzi wake akiwa na mwanamke mwengine.

Mboza lifikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida na hali yake inaendelea vizuri kwa matibabu.

"Jamani habari hii imepotoshwa si kweli kwamba amekufa yeye bado ni mzima na anaendelea vizuri na matibabu hospitali ya mkoa singida.ila uamuzi aliochukua sio sahahihi.asubuhi tulifika kumuona hospitali" Aliandika mtu mmoja kwenye blog fulani iliyoripoti kuwa binti huyo alifariki dunia siku iliyofuata baada ya tukio.

Katika jamii inafahamika kuwa vyuoni ni sehemu ambako wasomi na watu wenye kujitambua zaidi kutengenezwa. Lakini mambo yanaonekana kuwa ni tofauti kwa sababu huko vyuoni ndiko ambako kumekuwa kukiripotowa kutokea vitu vya ajabu kila kukicha.

 

 
Moza akiwa amelazwa kwenye kitanda cha Hospitali ya Singida muda mfupi baada ya Kufikishwa Hospitalini hapo.
 Kwa Matukio Mengine Ingia Hapa>>
 
Top