Kwa wale wenye mahusiano ya Kimapenzi ama Ndoa, Unaweza kubaini endapo Mwandani wako ana Mahusiano ya Kimapenzi na Mpenzi wake wa zamani (X wake) kwa kuangalia mambo haya nyeti;

Jambo la kwanza kabisa, ukiona mpenzi wako au mwana ndoa wako anamtaja X wake mara kwa mara iwe kwa mema ama kwa mabaya, ujue hapo kuna namna. Ni lazima mtu huyo atakuwa na hisia za kimapenzi kwa mtu wake huyo ambaye wewe unafikiri kuwa ni X wake. Kama na wewe una tabia hiyo acha mapema usije ukamtia mashaka Uliyekuwa naye kwa sasa.
  •  Pili ukiona mpenzi wako anamiliki namba za simu za  X wake basi ujue kuna namna tu. Kama wameachana namba za simu ni kwaajili ya nini? kuna ajenda gani ambayo inaendelea hadi aendelee kumiliki namba za huyo mtu wake wa zamani. Hakuna kitu cha namna hiyo kabisa, na ukiona hivyo anza kuwa na mashaka.
  •  Ukimuona Mwandani wako anashituka kila anapomuona X wake ujue kuna jambo hapo. Wakatiu mwingine hata unapokuwa naye umeshikana naye kimahaba, atakuachia na kama mna tembea atatangulia mbele na kujifanya kama vile haupo naye. Mwenzangu hapo kaa chonjo Bomu hilo.
  • Kama Mpenzi wako anajifanya kuwa na urafiki wa kawaida na X wake, kaa mkao wa kuibiwa ndugu yangu. Kama mtu mmeachana na kila mmoja akaangalia ustaarabu wake, huo urafiki wa kawaida ni wa nini? Hakunaga urafiki wa kawaida kwa mtu na mpenzi wake wa zamani. Ni rahisi sana kwa watu wa namna hiyo kukumbushia waliyokuwa wakifanya zamani. Usikubali kufanywa Bwege ndugu hakuna hali halisi ya namna hiyo. Hiyo ni dalili ya wizi, kaa 'Atensheni'.
  •  Unapoona Laazizi wako anaanzisha Ugomvi kila unapohoji kuhusiana na wasiwasi wako unaouona kati yake na X wake na wakati mwingine kutishia kuachana, hapo ujue nyuma ya pazia kumenoga. Hapendi uzungumzie suala hilo kwasababu anafahamu Kama ukihoji zaidi utaweza kubaini Ukweli, hivyo anajifanya kuwa mkali ili utakapoona dalili yoyote uogope kuhoji.
  • Anapopokea simu ya huyo X wake akiwa na wewe anajifanya hasikii na kuitikia kisha kukata simu na pengine kuzima kabisa. kwa mfano utamsikia akisema "Haloo....Halooo....Mbona sikusikii?" Kama kweli hakuna kinachoendelea kwanini asipokee na kuongea naye vizuri? Anajua mada zao hazitakupendeza na ndiyomaana anajifanya hasikii ili usiweze kusikiliza mazungumzo yao.
 Itaendelea Juma Tano

 
Top