Wenzake wanne watokomea kizani na kuacha simu zao mikononi mwa polisi baada ya mwenzao kujeruhiwa vibaya.
Mtu mmoja ambaye hajatambulika jina lake na anakotoka
amefariki dunia baada ya kulipukiwa na bomu huku utumbo wake ukiwa nje na mkono
wake kukatika alilotaka kuwarushia askari polisi waliokuwa doria usiku wa
kuamkia leo na kujeruhi askari polisi wawili ambao hali zao zinaendelea vizuri.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu ameiambia ITV kwa
njia ya simu kuwa watu wa nne waliokuwa na mtu huyo wamekimbia huku polisi
wakikamata simu za watu hao pamoja na ya marehemu huyo na kwamba hili ni tukio
la tatu la mabomu dhidi ya askari Polisi na amasema kukamatwa kwa simu hizo ni
mwanzo mzuri wa kuwabaini walipuaji mabomu kwa askari polisi mjini Songea.
Mkuu huyo amesema kuwa kutokana na uzito wa tukio hilo
mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini CP Isaya Mungulu anafanya safari kuja
Songea leo na atazungumza na vyombo vya habari.
Mwandishi wa habari hii aliyekuwepo eneo la tukio aliweza
kushuhudia mabaki ya bomu hilo pamoja na mzula wa kuziba sura
Chanzo: ITV