Tukio la kusikitisha limetokea katika nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo likiwaonesha wanajeshi kwa kushirikiana na wananchi wenye hasira kali kumuua kwa kumpiga vibaya mawe na vitu vyenye ncha kali kibaka mmoja alieiba begi.

Katika hali ya kushangaza wanajeshi hao wakiwa wamevalia sare zao za kijeshi walionekana wakijumuika na wananchi wenye hasira kali kwenye kumuua kibaka huyo, jambo ambalo watu walitegemea kuwa kwa uwepo wa wanajeshi hao pengine kibaka huyo asingepigwa na badala yake angeokolewa mikononi kwa raia wenye hasira kali na sheria ingechukua mkondo dhidi yake, lakini tukio lilienda ndivyo sivyo baada ya wanajeshi nao kuonekana kumchangia kibaka huyo pamoja na raia kwa kumpiga mpaka kumuua.

Tukio hili ambayo ilizua mzozo mkubwa nchini humo mpaka kufika kwa mkuu wa majeshi ambapo alisema "tukio hili ni la kisikitisha pia kulidhalilisha jeshi, hatua kali za kijeshi zitafuatwa kwa wanajeshi walioonekana kushiriki kwenye tukio hili". Pia aliendelea kusema wanajeshi hao watatafutwa mpaka wapatikane na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

 Hata hivyo wananchi wa nchi hiyo wameonekana kukosa imani na wanajeshi wao, kwani kwa tukio hilo baya walilolifanya limewaongezea hofu na kusisitiza nidhamu za kijeshi ziongezwe ili wanajeshi wajue majukumu yao ya nini la kufanya iwapo wataona kuna tukio baya limetokea katika eneo walilopo.
CRDT: Nyuma ya Pazia


 
Top