Mwanamke mmoja ambayE jina lake ni Nosma Dube mwenye umri wa miaka 28 amemchoma mumewe sehemu za siri kwa maji ya moto baada ya kuhisi akiwa anamsaliti na mwanamke mwingine

Mwanaume huyu ambaye jina lake ni Fezile Dubes (35) ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya uvimbe sehemu zake za siri na walipomfuata daktari aliwaambia kwamba mwanaume huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa hata wa mkanda wa jeshi a,bapo daktari alisisitiza mwanaume huyo kurudi baada ya miezi mitatu ili kuja kufanya vipimo vya ugonjwa wa Ukimwi baada ya miezi mitatu.

Baada ya kurudi nyumba mwanaume huyo alikiri kuwa na wasichana ambao alikuwa akilala nao nje ya ndoa yake, na mkewe baada ya kuambiwa hivyo alianza kumlaumu na kumuliza kwaninI hakutumia kinga.

Licha ya mwanaume kuwa na michepuko nje ya ndoa yake lakini ilikuwa tofauti kwa mkewe ambaye alikuwa muaminifu kwa mumewe ndipo alipokasirika na kumchoma na maji ya moto kwa mujibu wake anasema mumewe anabahati sana kutokana na kwamba hakumwambukiza laiti kama angelikuwa kamuambukiza basi angefanya kitendo cha kikatili zaidi ya kumchoma na maji ya moto mumewe. 

 
Top