Mabaki ya nyumba ya mzee ambayo ilichomwa kutokana na imani za kishirikina.
Mauaji haya hufanyika kikatili kwa kutumia mapanga, mawe, mashoka na kuwachomea nyumba.
Madai ya kuroga mvua, upigaji ramli, ugomvi ndani ya ndoa, tamaa ya kurithi mali, ardhi na ng’ombe ni miongoni mwa mambo yanayoelezwa kusababisha ongezeko la mauaji ya wazee vikongwe katika baadhi ya mikoa nchini.
     Shirika linalojishughulisha na haki za wazee la Help Age International, limetaja sababu hizo kuwa ndizo zilizoendeleza wimbi la mauaji hadi kufikia idadi ya wazee zaidi ya 4,612 kuuawa kutoka mwaka 1998 mpaka 2014.
      Anasema kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ya mwaka 2009, wanawake wazee 2,583 waliuawa katika mikoa minane ikiwa ni wastani wa mauaji 517 kila mwaka.
     “Takwimu za Mkoa wa Mwanza pekee, ambao ndiyo ulikuwa na mauaji mengi nchini zilionyesha kuwa wanawake wazee 689 waliuawa kati ya mwaka 2002 na 2007 ikiwa ni wastani wa mauaji 140 kila mwaka,” anasema Meneja wa Programu wa Help Age, Flavian Bifandimu.
      Anasema taarifa kutoka Shinyanga pia zinatisha, kwani wanawake wazee 242 waliuawa kati ya Januari 2010 na Juni 2011.

Sababu za mauaji
     Mwenyekiti Mtendaji kutoka asasi ya Maperele ya Magu, Joseph Mandalo anasema mauaji ya wazee Mwanza na maeneo yanayouzunguka mkoa, yalitokana na ugomvi wa kifamilia na ndoa.
    “Mauaji ya wazee yana sababu nyingi, mara nyingi yanaanzia katika migogoro ya familia na tatizo kubwa ni ardhi na mali. Sasa inapofikia hatua wanazihitaji, wanatumia kigezo cha kwamba ni mchawi ili wapate kirahisi,” anasema Mandalo.
      Anaongeza: “Wengi wanatumia njia za mkato kujipatia mali kwa kuondoa uhai wa wengine. Ukichunguza kwa umakini utagundua kwamba mipango ya mauaji inafanywa na wanafamilia.’’   Endelea>>
 
Top