
Ni
jambo linaloweza kuwa geni kidogo kwa baadhi ya makabila, lakini kwa baadhi ya
Wachaga wa Kilema mkoani Kilimanjaro kuna mila ambazo kwa makabila na jamii
nyingine zinaweza kuwa za kushangaza.
Jamii
hii inaonekana kuwa tofauti na Wachaga wengine kwani wao huwafukua wapendwa wao
waliofariki kila wanapotimiza miaka minane hadi 10 baada ya kuzikwa.
Mila
hiyo ina taratibu zake za kufuata kabla ya kufikia hatua ya mwili kufukuliwa
sehemu ulikokuwa umezikwa na kwenda kuhifadhiwa sehemu nyingine.
Kitendo
cha kufukua maiti kimekuwa kikifanywa kwa kufuata taratibu maalumu za kimila na
zisipofuatwa inaaminika huwa na madhara makubwa kwa ukoo ikiwamo kusababisha
kifo.
Mmoja
wa wanaukoo wa Lyimo, Edward Lyimo anasema utamaduni huo aliukuta tangu akiwa
mdogo na unaendelea mpaka sasa akiwa mtu mzima.
“Si
jambo la ajabu. Katika utu uzima wangu nimeshafukua ndugu zangu wengi tu
waliokufa miaka ya nyuma na kuihifadhi eneo maalumu lililotengwa na familia kwa
ajili hiyo,” anasema.