Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha
Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika
kijiji cha Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo.
Wananchi wa vitongoji vya Kazunzu, kijiji cha Nyambemba,
kata ya Kazunzu, wakishirikiana na wa kitongoji cha Lueseselo, kata ya
Bulyaheke, wamempiga kwa marungu, mawe
na mapanga na kisha kumchoma moto mtu ambaye bado hajafahamika, wakimtuhumu
kuwa wakala wa kuteka watoto wakiwamo walemavu wa ngozi (albino), akishirikiana
na waganga wa kienyeji wapiga ramli kwa imani za kishirikina za kupata utajiri.
Mbali ya kumuua, wananchi hao pia wamevunja na kuchoma moto
nyumba 13 zilizoezekwa kwa bati mali ya mganga wa kienyeji mwanamke mpiga ramli
mwenye umri wa miaka 40 (jina linahifadhiwa).
Hata hivyo, mganga huyo na familia yake walifanikiwa
kuwatoroka wananchi hao.
Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha
Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika
kijiji cha Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo.
Richard Mangalamu baba wa mwanafunzi aliyetekwa, Winfrida
(11) anayesoma darasa la nne Shule ya Msingi Kazunzu, alisema mtuhumiwa
alimwachia mwanafunzi huyo kutokana na kumkuta ana chale mgongoni na kifuani
akidai amepoteza ubora.
Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Wilaya ya Sengerema, Babu Sanare
na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Enock Mabula, kwa nyakati tofauti
walithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Naye Diwani wa Bulyaheke, Bagadi Nyuki, akiwa eneo la tukio,
alisema chanzo cha mauaji hayo ni marehemu kudaiwa kuwa juzi alimteka mwanafunzi
wa kike anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Kazunzu na kumvutia
vichakani na kisha kumvua nguo na kumpapasa.
Inadaiwa kuwa alimuachia huru baada ya kugundua kuwa hakuwa
na sifa zinazohitajika na mganga na mwanafunzi huyo alipofika nyumbani
aliwaeleza wazazi wake na ndipo wakishirikiana na wanakijiji wenzao walianza
kumsaka mtuhumiwa na kufanikiwa kumtambua.
Inadaiwa baada ya kubanwa mtuhumiwa huyo alikiri na
kujitambulisha alikuwa ametoka kijiji cha Katoro, mkoani Geita na alikwenda
Sengerema kwa kazi ya uwakala wa kuteka watoto.
Diwani huyo alisema marehemu aliomba apelekwe kijiji jirani
cha Bulyaheke umbali wa kilometa sita kutoka Kazunzu kwa mwenyeji wake na mdau
mwenzake, Sato, lakini wapofika walikuta amekwisha kutoroka.
Wakati huohuo, mwili wa mtoto Yohana Bahati aliyeuawa kwa
kukatwa miguu na mikono, mwili wake utazikwa kesho katika kijiji cha Kataro,
mkoani Geita.
CHANZO NIPASHE