Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema watu wote wanaopanga kubaki katika vituo vya kupigia kura baada ya kumaliza kwa zoezi hilo kwa lengo la kulinda kura kuna ashiria uvunjaji wa amani, hivyo serikali imejipanga kupambana na hali hiyo wakati wa uchaguzi.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh Jakaya Mrisho Kikwete
Rais amesisitiza kuwa wanaopaswa kulinda kura ni mawakala pekee na si wafuasi wa chama ama mpiga kura.

Akizungumza katika sherehe za kilele cha mbio za mwenge wa uhuru zilizofanyika kwenye uwanja wa jamhuri mjini Dodoma, kiongozi huyo anayemalizia muda wake madarakani amesema viongozi wanaowaagiza wanachama wao kulinda kura wana nia mbaya na amani ya nchi.

"Mnatakiwa muondoke kwenye vituo baada ya kupiga kura......kura utazilindaje? Mawakala ndio pekee wanaolinda. Mkikaidi hilo, hatutawavumilia. Serikali imejipanga kupambana na wale wote watakaokaidi agizo la tume ya uchaguzi (NEC) Amesema Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Chanzo: Mwananchi

 
Top