Mtayarishaji wa vipindi, Sospeter Jonas amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Dodoma Mjini akishitakiwa kwa matumizi mabaya ya mtandao.
Sospiter
alisomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mussa mbele ya Hakimu
wa Mahakama hiyo Emmanuel Bwile.
Mshtakiwa
huyo anadaiwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook ujumbe kuwa “Pinda
utakuwa muhubiri wa injili tu.”
Mussa
aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa huyo alibandika picha ya John Maliga kwenye
ukurasa wake wa Facebook na kuandika ujumbe huo, kitendo ambacho ni kinyume cha
kifungu namba 16 cha Sheria ya Mtandao ya Mwaka 2015.
Mlalamikaji
katika shauri hilo la jinai namba 815/2015 litakalokuja tena mahakamani Oktoba
19, ni John Maliga.
Mshtakiwa
yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana iliyomtaka kuwa na mdhamini
mmoja na bondi ya Sh1 milioni.
Kesi hii
imekuja baada ya wiki iliyopita, kijana mmoja, Benedict Ngonyani (24) kufikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akituhumiwa kusambaza
taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis
Mwamunyange.
Kijana
huyo anatuhumiwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook na WhatsApp kuwa,
Mwamunyange, amelazwa kwenye hospitali moja mjini Nairobi, Kenya kwa madai ya
kulishwa chakula chenye sumu.
Chanzo: Mwananchi