Kamanda wa Polisi mkoani kilimanjaro Flugence Ngonyani
Kigogo mmoja wa CCM wilayani Rombo anadaiwa kumnajisi mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.
Mama mzazi wa mtoto huyo alidai kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 17, usiku nyumbani kwao Mwanga walipokuwa wamelala na alishtuka baada ya kusikia sauti ya mtoto akilia kutokea chumba kingine.
"Nilipoamka nilikwenda hadi kwenye kile chumba na kumkuta mwanangu anatokwa na damu sehemu za siri. Nilimchukua na kumpeleka kituo cha afya cha Mwanga" alidai mama huyo.
Alidai kuwa daktari aliyemtibu alithibitisha kuwa alikuwa amenajisiwa
Hata hivyo alidai kuwa baada ya mumewe kufanya kitendo hicho, alikwenda kwenye kituo chake alichokuwa anafanyia kazi alichohamishiwa hivi karibuni wilayani Rombo.
"Tangu amefanya kitendo hiki, hajawasiliana na mimi na tayari nimeshafungua jalada polisi, nadhani alidhamiria kufanya kitendo hiki, amemuumiza mtoto" alidai mama huyo.
Kamanda wa Polisi mkoani kilimanjaro Flugence Ngonyani alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa mtuhumiwa anatafutwa na polisi ili afunguliwe shitaka la ubakaji.
MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>
MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>