Katika
siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa
za uzushi na uongo kutumia majina ya taasisi, mashirika ya umma na ofisi
za Serikali na kueneza taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kwa
lengo la kupotosha wananchi.
Miongoni
mwa taarifa hizo ni pamoja na taarifa kuhusu Jeshi la Polisi
iliyosambazwa jana katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari
‘chujio Jesho la polisi, vyeti feki vyawaonndoa askari kazini’ Taarifa
hiyo ni uzushi na haijatolewa na Jeshi la Polisi.
Kufutia
hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapenda kukanusha taarifa hiyo ya
uzushi ambayo haina ukweli wowote na inalengo la kuchafua taswira ya
Jeshi la Polisi kwa jamii.
Jeshi
la Polisi nchini limeanza upelelezi wa kuwatafuta watu wote waliohusika
kueneza taarifa hiyo na kujifanya wao ni Jeshi la Polisi.
Aidha, Tunatoa onyo kali kwa watu wote kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kufanya uposhaji na badala yake watumie mitandao hiyo kwa ajili ya ustawi wa jamii.
Aidha, Tunatoa onyo kali kwa watu wote kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kufanya uposhaji na badala yake watumie mitandao hiyo kwa ajili ya ustawi wa jamii.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>