MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu kifungo cha maisha jela,
Siasa Mwinyi (40) baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mtoto wa
miaka tisa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili. Hakimu Mkazi
Mwandamizi, Juma Hassan alisema Mahakama imeridhishwa na yaliyoelezwa na
mashahidi wanne.
Mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari mwaka huu katika eneo la Tabata
Kisukuru katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam. “Makosa ya ukatili
yamekuwa ni mengi na hatujui tatizo ni nini kwa sababu kila kukicha
watoto wanafanyiwa ukatili na unyama wa namna hii na mambo kama haya
yanapaswa kulaaniwa na kila mtu,” alisema hakimu huyo.
Kwa mujibu wa hakimu, ushahidi uliotolewa na mtoto huyo ambaye ni
mwanafunzi wa shule ya msingi Magoza iliyopo Tabata Segerea, Mwinyi
alikuwa akimwingilia kila mara wakati alipokwenda nyumbani kwa
mshitakiwa huyo kunywa maji.
Alidai mshitakiwa alikuwa akimnajisi mtoto huyo mara kwa mara katika
migomba wakati akitoka shuleni na watoto wenzake. Kabla ya kutolewa kwa
hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Agatha Lumato aliiomba mahakama hiyo
kutoa adhabu kali dhidi ya mshitakiwa huyo kutokana na kukithiri kwa
vitendo hivyo.
Hata hivyo, Mahakama ilitoa nafasi kwa mshitakiwa aeleze kwa nini
asihukumiwe ambapo alijitetea kwa kuiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa
sababu ana mke na watoto watano wanaomtegemea na pia hajui kusoma wala
kuandika.
MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>