Mamake Farzana akiomboleza kifo cha mwanawe
Mwanamke mmoja nchini Pakistan amepigwa mawe na familia yake
wakiwemo babake na ndugu zake wa kiume hadi kufariki. Aliuawa nje ya jengo la
mahakama mjini Lahore.
Mwanamke huyo aliuawa kwa kuolewa na mtu ambaye alikuwa
chaguo lake mwenyewe.
Farzana Bibi, mwenye umri wa miaka 31, aliolewa na Muhammad
Iqbal miezi michache iliyopita bila ya idhini ya familia yake.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alishambuliwa na familia
yake.
Kaka zake na binamu yake mmoja walimshika alipokuwa akiingia
mahakamani na kuanza kumpigwa kwa mawe . Alifariki popo hapo.
Waliomuua walikimbia kabla ya polisi kufika katika eneo
hilo.
Babake msichana huyo amekamatwa ingawa washukiwa wengine
wangali hawajulikani waliko.
Kwa wanawake wanaoolewa na wapenzi ambao ni chaguo lao
wenyewe, ni kitendo kisichokubalika kitamaduni katika baadhi ya maeneo ya
Pakistan.
Mamia ya wasichana huuawa kwa kisingizio cha kuolewa na watu
wasiokubalika na familia zao kila mwaka
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wanaamini kuwa kwa
kuwa mauaji hayo hufanywa na familia zenyewe, huwa ni vigumu kufikisha kesi
hizo kortini.