Imeandikwa Na: Farid Mugasa Kutoka Geita.
Mwanamke anayesadikiwa kuwa mchawi na anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka kati ya 29-35, Mchangani mkoani Geita wilaya ya Sengerema, amekutwa amelala nje ya nyumba moja majira saa tatu za usiku huku akiwa na kipande cha ngozi ya mnyama mwilini na kichwani amejifunga vitambaa viwili, cheusi na chekundu.
Mwanamke anayesadikiwa kuwa mchawi na anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka kati ya 29-35, Mchangani mkoani Geita wilaya ya Sengerema, amekutwa amelala nje ya nyumba moja majira saa tatu za usiku huku akiwa na kipande cha ngozi ya mnyama mwilini na kichwani amejifunga vitambaa viwili, cheusi na chekundu.
Pia mwanamke huyo alikutwa na kibuyu kinachodhaniwa kuwa ni moja kati ya dhana za kichawi, kikiwa pembeni yake pamoja na simu ya mkononi na vocha iliyokwisha kutumika. Nguo za mwanamke huyo zilikuwa pembeni jambo ambalo linatoa ishara kuwa alivua kwaajili ya kufanya shughuli yake inayosemekana kuwa ni ya kichawi.
Habari kamili inasemekana kuwa Mwenye nyumba ambayo mchawi huyo alidondoka, alishikiliwa na polisi kwaajili ya kutoa ushirikiano wa uchunguzi wa kifo cha mtu huyo.
Kwa maelezo ya mwenye nyumba huyo, alisema kuwa kutokana na mtoto wao kuugua na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji, waliambiwa kuwa kuna watu ambao walikuwa wakimchezea mtoto huyo na madhumuni yao yalikuwa ni kumuua.
Hivyo mganga alitoa matibabu kwa mtoto huyo kisha akawaambia kuwa wachawi hao waliokuwa wanamroga mtoto huyo walidhamiria kufanya hivyo. Kwahiyo mganga aliwapa dawa na kuwaambia kuwa wachawi hao wangekwenda nyumbani kwa mtoto huyo na kuendelea kumfanyia mambo ya kichawi.
Mganga aliwapa dawa na kuwaambia usiku wa siku hiyo walitakiwa walale mapema sana kwasababu wachawi wangefika nyumbani hapo kuendelea na kamchezo kao.
Baada ya kurudi nyumbani mwenyenyumba alisema kuwa ilipofika majira ya saa tatu usiku walilala kutokana na maelezo na masharti waliyokuwa wamepewa na mganga wao.
Walipoamka asubuhi ndipo wakamkuta mwanamke huyo akiwa amelala chini huku tayari amekwisha kupoteza maisha. Kwa namna hiyo waliamini kuwa mwanamke huyo ambaye alikuwa uchi na nguo zake zikiwa pembeni ni miongoni mwa watu waliokuwa wakimchezea kijana wao.
Askari waliuchukua mwili wa mwanamke huyo anayesadikiwa kuwa ni mchawi pamoja na mwenye nyumba na kwenda nao kwenye kituo cha polisi kwaajili ya uchunguzi zaidi. Na mganga ambaye alihusika na zoezi la kuzindika nyumba hiyo anasakwa na polisi.
_______________________________________________________________________________________