Kijana mwenye umri wa miaka 13 aliyefahamika kwa majina Karume Kauzu Habibu, amekamatwa leo mjini Morogoro katika hospitali ya mkoa kwa tuhuma za kujifanya Daktari. 


Inasemekana kijana huyo amekamatwa baada ya muuguzi mmoja kutoa ripoti kwa kuhisi kumshuku kijana huyo kuwa hakuwa Daktari kama wengi walivyokuwa wakimdhania. Baada ya askari kumfuatilia, walibaini ni kweli Bwana habibu hakuwa Daktari na alikuwa akijifanya Daktari kwa kuvalia koti refu jeipe ambalo huvaliwa na madaktari.

Chanzo chetu cha habari kimeendelea kuripoti kuwa, Habibu alikuwa akiingia hospitalini hapo huku akiwa amevalia vazi hilo lililofanana na vazi la Daktari kwa takribani wiki tatu sasa huku watu wakiamini ni kweli alikuwa ni daktari halali wa hospitali hiyo, na hata baadhi ya watu wakiwemo baadhi ya wauguzi na wagonjwa walikwisha anza kumzoea.

Baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo alikutwa na vitambulisho vitatu tofauti, huku kimoja kikionesha kuwa anarudia mtihani katika kituo kimoja hapo mjini Morogoro, alikuwa ni mwenyeji wa mkoani Kigoma, na kwa wakati huu alikuwa akiishi maeneo ya Liti mkoani humo.

Kwa maelezo ya Dk. Fransic Semwene ameeleza kuwa Daktari huyo feki hakusababisha madhara yoyote katika kipindi chote alichokuwepo hospitalini hapo. Alichokuwa akikifanya ni kuwaagiza wahudumu kutoa huduma kwa wagonjwa kwa haraka. Na alipo hojiwa alieleza kuwa aliamua kuvaa mavazi ya kidaktari ili kuweza kuingia hospitalini hapo pasipo kikwazo, na alichokuwa akikifuata hospitalini humo ni kutoa huduma kwa ndugu zake.

Hadi sasa askari wa jeshi la polisi wamemshikilia kijana huyo na kuendelea na uchunguzi, ili kuweza kuzuia tabia kama hiyo ya udanganyifu.


 
Top