Soko la Sarafina - Jamatini mkoani Dodoma limeungua moto na kusababisha hasara kubwa ambayo haikuweza kufahamika kirahisi. Moto huwo ambao ulizuka jana usiku majira ya saa tano, uliweza kusababisha vibanda zaidi ya 63 kuteketea.
Moto huwo ambao chanzo chake hakikuweza kufahamika, ulileta changamoto kwa jeshi la kuzima moto kutokana na kutokuwa na njia ambazo magari ya kuzimia moto yangeweza kufika kwa urahisi. Hata hivyo jitihada za jeshi hilo ziliweza kuzaa matunda baada ya lisaa limoja ambapo walifanikiwa kufika katika eneo la tukio na kuendelea na zoei la kuzima moto huwo na kujaribu kuokoa baadhi ya vitu.
Pamoja na jitihada zilizofanywa na wananchi pamoja na jeshi la kuzima moto kuwa kubwa, lakini moto huwo uliweza kuteketeza vibanda zaidi ya 63, na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.
Wafanya biashara wa soko hilo la Sarafina wakiutazama kwa masikitiko makubwa moto uliokuwa ukiteketeza mali zao usiku wa jana.
Baadhi ya wananchi wa mjini Dodoma wakijaribu kuzima moto katika soko la Jamatini mjini humo.
Wanajeshi wa zimamoto wakiendelea na zoezi la kuuzima moto huwo baada ya kufanikiwa kufika kwa taabu katika eneo la tukio kutokana na kukosekana kwa miundombinu.