Taarifa za kuficha watoto katika mazingira magumu imesababisha watu wa mkoa wa Morogoro kupewa hila hiyo ambayo si njema. Jambo hili limetokea kutokana na mfurulizo wa matukio yanayofanana kutokea katika mkoa huwo.


Miezi michache iliyopita kuliripotiwa mtoto kufichwa kwa mtoto (Nasra Mvungi) kwenye boksi kwa takribani miaka mitatu pasipo kupewa huduma muhimu zikiwemo chakula bora na huduma za afya.

Hivi sasa kumeripotiwa tukio jingine linalofanana kabisa na tukio lililokuwa limetokea katika manispaa ya Morogoro, ambapo katika kijiji cha Matongola, tarafa ya Magole wilayani Kilosa, kumebainika mtoto mwenye umri wa miaka sita Devotha Malole, kufichwa chini ya uvungu na mama yake mzazi anayefahamika kwa jina la Sara Mazengo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa hizo ziliripotiwa Siku ya Ijumaa majira ya mchana katika kituo cha polisi, baada ya uongozi wa kijiji na kata kutoa taarifa. Mwanamke huyo anayetuhumiwa kufanya ukatili huwo ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na kuweza kubaini sababu za mtoto Devotha kufichwa chini ya uvungu kwa kipindi chote hicho.
 
Top