Bwana mmoja ajulikanae kwa jina la Lack (32) mkoani Mara katika wilaya ya Butiama, amejikuta akipoteza mke baada ya baba yake mzazi kumgomea mke wake kuingia ndani siku ya harusi.


Chanzo cha habari hizi kimesema kuwa, Sakata hilo lilianza nyumbani kwa mwanamke majira ya saa tisa za jioni baada ya kufunga ndoa ya kimila. 

Chanzo chetu kimeendeleza kueleza kuwa, bwana harusi (Lacky) alishindwa kufika kwenye harusi siku hiyo kutokana na kuwa safarini mkoani Arusha kikazi. Hivyo alitafuta mtu wa kwenda kufunga ndoa kwa niaba yake.

Sakata lilianza baada ya kufunga ndoa hiyo, yule aliyepewa jukumu la kuoa kwa niaba ya Laky, pamoja na ndugu wa mume walikwenda nyumbani kwa mwanamke kwa lengo la kumchukua mke wao na kuondoka naye. Walipofika nyumbani hapo walimkuta baba wa bibi harusi ameketi karibu na mlango wa kuingilia ndani, hivyo wageni wale ikabidi wakamsalimie ndipo waingie ndani kumchukua mke wao.

Mzee yule aliposalimiwa na wakwe zake kwa heshima, aligeuza shingo yake na kutazama pembeni. Kitendo kile kiliashiria kuwa baba yule asingeitikia salamu zao hadi apatiwe pesa. Ndipo jamaa aliyekuwa amepewa jukumu la kuoa alipozama mfukoni na kuibuka na noti ya shilingi 5,000/=. Hapo baba wa bibi harusi ndipo alipopokea na kuitikia salamu za wakwe zake.

Bibi harusi (Anna) aliondoka na pamoja na watu wale majira ya saa kumi na mbili za jioni kuelekea kijiji cha jirani ambako ndiko baba yake Lacky alipokuwa akiishi.

Kama ilivyokuwa imetokea nyumbani kwa mke (Anna), ndivyo ilivyokuja kutokea nyumbani kwa mwanamume. walimkuta baba yake Lacky ameketi katikati ya mlango. Lengo lilikuwa ni lile lile la kutolewa pesa ndipo maharusi wale waingie ndani. Ingawa kulikuwa na utofauti kidogo, kwani baba Lacky alihitaji shilingi 10,000/= ndipo amruhusu mke wa kijana wake kuingia ndani.

Ndugu wa mwanamke ambao walikuwa wamemsindikiza binti yao kwa mume wake, walikwama baada ya kukosa kiasi kile cha pesa. Ilibidi watu wa pande zote mbili wajichange change na kuibuka na kiasi cha shilingi 8,500/= tu. walimpigia magoti mzee yule lakini ilikuwa vigumu kupokelewa kiasi kile cha pesa.

Vuta nikuvute iliendelea hadi majira ya saa tano za usiku, baba Laky hakukubaliana kabisa na kitendo cha kumruhusu mke wa kijana wake kuingia ndani pasipo kutoa kiasi kile cha pesa alichokuwa amekitaka yeye. 

Ndugu wa bibi harusi walikasirika na kumchukua binti yao na kuanza kurejea nae nyumbani kwa miguu usiku ule wa saa sita pasipo usafiri wowote pamoja na kwamba kuna umbali mrefu.


 
Top