Manamke mmoja Ruqiya Farah Yarow, nchini Somalia katika mji wa Hosingo ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa ni wanamgambo wa kundi la kiislamu la Alshabab.


Kwa mujibu wa wanandugu wamezungumza na chombo kimoja cha habari na kueleza kuwa ndugu yao huyo alikuwa amepewa amri ya kujisitiri kwa kuvaa hijabu kuambatana na sheria za kiislamu, lakini mwanamke huyo alikaidi.

Ndugu wa Ruqiya Farah Yarow, wamezungumza na chombo hicho cha habari na kusema kuwa ndugu yao huyo aliwafukuza wanamgambo wa kundi hilo, wakati walipomfuata nyumbani kwake kwaajili ya kumshinikiza kujifunika kichwa chake. Aliwaambia waondoke nyumbani kwake kwani angefanya watakavyo baadae.

Wanamgambo hao waliondoka, na kurudi tena baadae ambapo walimkuta Ruqiya akiwa hajafunika kichwa chake. Hapo ndipo walipotoa bunduki na kumuua hapo hapo kwa kumpiga risasi.

Hata hivyo msemaji wa kundi hilo la Alshabab amekanusha kuhusika na mauaji ya mwanamke huyo kama ambavyo imedaiwa.

Jiunge hapa Kwenye ukurasa wetu wa Facebook Tukuhabarishe kila siku >> 

 
Top