Ni ajali mbaya sana ambayo imepelekea zoezi la kubaini miili ya marehemu kuwa gumu kutokana na miili hiyo kujeruhiwa vibaya.
Watu 12 wameripotiwa kufariki dunia na miili yao kuharibika vibaya baada ya ajali ya basi
dogo kugongana uso kwa uso na Lori la mafuta katika eneo la Makumira wilayani
Arumeru jijini Arusha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Libaratus Sabas
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali hiyo imetokea leo majira
ya saa kumi jioni ambapo daladala hiyo iliacha njia yake na kwenda kulivaa Lori
lenye namba za usajili T582 ACR na kugongana uso kwa uso.
Walionusurika katika ajali hiyo ni watu wawili akiwemo mtoto
mdogo pamoja na dereva wa daladala hiyo ambaye alikimbia mara tu baada ya kutokea
kwa ajali.
Majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya Tengeru na miili ya
marehemu imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mount Meru jijini humo.
INNALILAHI WAINNA ILLAIHI RAJIUN – BWANA ALITOA BWANA
AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.