Nasib Abdul "Diamond Plutnumz"
Baada ya kutolewa tangazo la Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasib Abdul maarufu kama Diamond Plutnumz kutunukiwa PHD na chuo kikuu cha Mlimani, kumezuka mitazamo tofauti kutoka kwa wananchi.
Utamu wa Raha imefanikiwa kupitia baadhi ya maoni ya wananchi kwenye baadhi ya mitandao na kukumbana na ujumbe kama ufuatao.
TANGAZO NGUGU ZANGU: Ifikapo Tarehe 8 Novemba Saa 10 jioni,Kijana
mwenzetu ambaye sisi tunamdharau na wengine wapuuzi kabisa kwa kufeli kwao
maisha wana wivu na wanathubutu kumzomea atakuwa anatunukiwa Shahada ya
Uzamivu(Phd) na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam(UDSM) kwa kuthamini mchango wake
kwenye jamii…Honorary Phd hata Raisi wetu anayo…Alongside DIAMOND mwingine
atakayepewa Shahada hii ya Heshima kwenye Mahafali haya ni Balozi Fulgence
Kazaura ambaye amewahi kuwa VC wa UDSM miaka ya nyuma!! Ningependa
kuwakaribisha wale Wazomeaji woooteee wenye sauti mbaha kabisa waweze kufika
kwenye Viwanja vya UDSM kushuhudia Tukio la Kihistoria kwa Mtoto huyu wa
Tandale ambaye ni BIDII NA HESHIMA Vimemfikisha hapa.. SHKAMOO DR.NASIBU ABDUL
au Pengine DR.DIAMOND PLATNUMZ au ukitaka swaga DR.PLATNUMZ BABY! Sky is never
the limit!Hongera kwa Mameneja waliomfikisha DIAMOND hapo alipo.
Mtandao mwingine ulinukuliwa ukiwa umeandika kama ifuatavyo:
Watafiti wa mambo wanakwambia phd ambayo atatunukiwa diamond
siku si nyingi zijazo ni ujanja ujanja wa msanii huyo. chanzo kimedai kuwa
msanii huyo baada ya kusikia mwenzake wa kundi la weusi aitwaye nicki wa
pili ametangaza kusomea phd siku chache zijazo. na kuonekana kuwa atakua
ndiye msanii wa kwanza kuwa DR. kwa bongo. diamond ameamua kufanya magumashi
ambayo kwa bongo hakuna kinachoshindikana ilmradi tu apewe sifa hiyo na kuweza
kuweka historia bongo. chanzo kingine kimefunguka na kudai kuwa ni ujanja wa
fiamond hili kujisafisha kwa watanzania na kumpoteza alikiba ambaye smeonekana
kuwa tishio maisha ya kimziki ya diamond.