Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekanusha uvumi kuhusu
kumtunuku msanii Diamond Platnumz shahada ya uzamivu (PhD) katika mahafali yake
ya 44 yatakayofanyika Mlimani City, Novemba 8 jijini Dar es Salaam.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimekanusha ujumbe
uliopo katika mitandao ya kijamii ambao unadai kuwa msanii wa kizazi kipya
Naseeb Abdul maarufu kama Diamond atatunukiwa Shahada ya Uzamivu ya heshima
katika mahafali ya 44 yanayotarajiwa kufanyika Novemba 8.
Ujumbe huo ambao ulieleza kuwa Diamond atakabidhiwa shahada
hiyo sawa na aliyekuwa mkuu wa chuo hicho marehemu Balozi Fulgence Kazaura
katikati mahafali yatakayofanyika katikati ukumbi wa Mlimani City.
Akizungumzia habari hiyo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Yunus Mgaya alisema hakuna kitu kitu kama
hicho – ni uzushi.
Chanzo IZZY TZ