Jeshi la polisi Njombe likitoa kichapo kwa wanafunzi
wa Njombe sekondari school (NJOSS)
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Njombe (NJOSS) wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kuchoma moto shule yao.
Kwa
mujibu wa mkuu wa shule hiyo: Mwalimu Benard William amesema kuwa
huenda chanzo cha tukio hilo kikaendana na uamuzi uliofanywa na bodi ya
shule hiyo ambayo ilikutana Oktoba 7 mwaka huu na kuadhimia
kuwasimamisha shule wanafunzi waliokuwa wametoroka shuleni usiku na
kwenda Disco. Akamalizia kwa kusema kuwa hata hivyo Uchunguzi wa tukio
hilo bado unaendelea.
Kamishna
wa elimu nchini ameifunga shule ya Njombe (NJOSS) kwa kipindi cha mwezi
mmoja kufuatia vurugu hizo zilizopelekea uharibifu mkubwa wa mali
zinazokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi za kitanzania Milioni moja.
Afisa
elimu shule za sekondari mkoani Njombe Said Nyasiro amesema kwa
wanafunzi hao wanatakiwa kurejea shuleni hapo baada ya mwezi mmoja
wakiwa na wazazi wao pamoja na pesa kiasi cha shilingi Lakimoja na Nusu
kila mmoja kwaajili ya kufidia mali zilizoharibika.
Hata
hivyo jeshi la polisi mkoani Njombe limefanikiwa kuwashikilia baadhi ya
wanafunzi kuhusishwa na chanzo cha vurugu hizo, huku wengine
wakisurubiwa vikali, kama wanavyoonekana kwenye picha.
Baadhi ya wanafunzi wa Njombe sekondari wakipokea kichapo kutoka kwa Jeshi la polisi
_________________________________________________________________________________