Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz'
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akisubiri zamu yake kupanda jukwaani
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya jeshi la polisi, baada ya jeshi kutoa tamko kuwa ni kinyume cha sheria, juzi Diamond alitakiwa kwenda kujisalimisha polisi lakini hakufanya hivyo jambo lililosababisha wenzake kukamatwa na kuwekwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Oysterbay, Kinondoni jijini Dar.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya jeshi la polisi, baada ya jeshi kutoa tamko kuwa ni kinyume cha sheria, juzi Diamond alitakiwa kwenda kujisalimisha polisi lakini hakufanya hivyo jambo lililosababisha wenzake kukamatwa na kuwekwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Oysterbay, Kinondoni jijini Dar.
Ilisemekana
kwamba baada ya Wasafi (madensa wa Diamond) kukamatwa, Babu Tale naye
alifikishwa katika kituo hicho ambapo maafisa kadhaa wa jeshi la polisi
walionekana katika eneo hilo wakiweka ulinzi mkali.
Diamond akiendelea kutoa burudani jukwaani
Ilielezwa kwamba wanaomsaka Diamond na waliowakamata Wasafi ni wanajeshi wa Military Police (MP) ambao waliwabwaga jamaa hao kituoni hapo kisha kuendelea na mambo yao.
Ilielezwa kwamba wanaomsaka Diamond na waliowakamata Wasafi ni wanajeshi wa Military Police (MP) ambao waliwabwaga jamaa hao kituoni hapo kisha kuendelea na mambo yao.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar, Camillus Wambura alisema bado
hajawasiliana na kituo cha Oysterbay kuhusu suala hilo na hajapata taarifa kwa
kuwa kesi hiyo inachunguzwa na iko chini ya Mkuu wa upelelezi wa Mkoa.
Akijibu kuhusu taarifa za uongozi wa Diamond na Diamond
kupewa muda wa kujieleza, Kamanda Wambura alijibu:
Chanzo hicho
kilieleza kwamba, siku ya tukio Oktoba 21, mwaka huu, uongozi wa Diamond
ulipewa muda wa kujieleza kabla ya saa 2:00 asubuhi lakini haukufanya hivyo
ndipo hatua hiyo ikachukuliwa.
Hata hivyo,
baadhi ya watu walikuwa wakihoji kwa nini jeshi la polisi lilimshikilia Babu
Tale peke yake bila Diamond lakini vyanzo vilieleza kuwa mwanamuziki huyo
huenda alikuwa safarini.
Alisema kosa la Diamond ni
kushindwa kutii wito kwani alitakiwa kuripoti mwenyewe polisi hivyo lazima
atapanda mahakamani kujibu shitaka hilo na lile lenyewe la kutumia sare za
jeshi hilo.Chanzo hicho kilidai kwamba si mara ya kwanza kwa jamaa huyo kuingia
kwenye kashikashi kama hiyo kwani kuna kipindi alikwenda Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo alionekana na sare hizo stejini na akapewa
onyo lakini safari hii amejiongeza tena kuonesha kuwa ni kichwa ngumu.
Diamond na Chege wakifanya yao
“Uchunguzi
unafanywa huko (Oysterbay). Kwa sasa hivi sina taarifa hiyo nina mambo mengi
sana. Kwa hiyo kwa sasa hivi uchunguzi unafanywa chini ya Mkuu wa Upelelezi wa
Mkoa. Sijapata nafasi ya kujua wamefikia wapi katika uchunguzi wa suala hilo.”
Mapema
wiki hii, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lilitoa taarifa kwa vyombo vya
habari likipiga marufuku raia kuvaa sare za jeshi.
Kwa
mujibu wa mwanajeshi wa JWTZ ambaye aliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji
wa jeshi hilo, taaluma yake ya sheria imemfanya kuchimba kwa undani suala hilo
na kugundua kuwa endapo Diamond atapatikana na hatia atapigwa faini au kwenda
jela miaka miwili au mitatu au vyote, yaani faini na kifungo.
___________________________________________________________________________________