Mama aliyetambulika kwa jina la Swaumu Sadick (25), mkazi wa Manzese jijini Dar, amejikuta yeye na manesi wakitimua mbio kwa woga baada ya kujifungua kiumbe wa ajabu.



“Nilimpa kitanda. Saa 8:00 usiku,  uchungu ulizidi nikampeleka leba ambako alijifungua kiumbe huyo mwenye jinsi ya kiume. “Baada ya kujifungua na kumuona kiumbe huyu wa ajabu, nilitimua mbio usiku huo kwa woga na kwenda kuamsha manesi wenzangu wanoishi kota za kituo hiki cha afya.

“Nimefanya kazi hii ya ukunga na kuzalisha wazazi zaidi ya 50 lakini sijawahi kukutana na tukio 
 

 
Swaumu Sadik akiwa hospitali baada ya kujifungua mtoto huyo

“Nilimpa kitanda. Saa 8:00 usiku,  uchungu ulizidi nikampeleka leba ambako alijifungua kiumbe huyo mwenye jinsi ya kiume. “Baada ya kujifungua na kumuona kiumbe huyu wa ajabu, nilitimua mbio usiku huo kwa woga na kwenda kuamsha manesi wenzangu wanoishi kota za kituo hiki cha afya.

“Nimefanya kazi hii ya ukunga na kuzalisha wazazi zaidi ya 50 lakini sijawahi kukutana na tukio kama hili.”

Kwa upande wake mganga mkuu wa kituo hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Dk. Beatrice alikuwa na haya ya kusema juu ya tukio hilo la kusikitisha:

“Kimsingi si kiumbe ila ni mtoto ambaye awali tulipomcheki mzazi tulibaini ana kichwa kikubwa na alishafia tumboni zaidi ya siku tatu.

“Amezaliwa akiwa na miezi nane tumboni. Tulichokifanya ni kuokoa maisha ya mama jambo ambalo tumefanikiwa.”


  
Swaumu Sadick akiuguzwa Hospitalini

Akizungumza kwa tabu na mwanahabari wetu, Swaumu alisema: “Hii ni mimba yangu ya tatu, ya kwanza iliharibika tumboni, ya pili nilifanikiwa kuzaa salama mwanangu Maimuna.
“Hii ya tatu ndiyo nimejifungua kitu hiki cha ajabu.”

Alipoulizwa kwa nini aliondoka Dar ambako ndiko kwenye hospitali kubwa na kwenda kujifungulia kijiji akijua ana matatizo ya uzazi, mama huyo alisema:
“Siku za kujifungua zilipokaribia mume wangu Abdallah aliniambia nije kujifungulia kwa bibi yangu Halima, kwa bahati mbaya ndiyo yametokea haya.”

Kwa upande wake shangazi wa Swaumu aliyekutwa akimhudumia alisema: “Yameshatokea ya kutokea, tunamshukuru Mungu na tunajiandaa kumchukua mjukuu wetu tukamzike.”
  
Mtoto wa ajabu aliyezaliwa na Swaumu




 
Top