Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha ACP
Liberatus Sabas.
Mwanamke
mmoja mkazi wa kijiji cha Olkokola Wilayani Arumeru Mkoani Arusha amefanyiwa
ukatili wa kutisha kwa kukatwakatwa na Panga kichwani na kuondolewa kiganja cha
Mkono, sikio na sehemu nyingine za mwili wake
Mwanamke
huyo anayefahamika kwa jina la Paulina Joseph amefanyiwa ukatili huo na mtu
anayedaiwa kuwa ni shemeji yake kwa madai ya kuingilia ndoa yake.
Tukio hilo
lilimkuta Bi Paulina akiwa shambani kwake akikata nyasi kwa ajili ya kulisha
mifugo.
Mume wa
Paulina ameeleza masikitiko yake kwa uongozi wa kijiji,Kitongoji na kata kwa
kushindwa kumkamata mtuhumiwa na kutoroka kwani kitendo hicho kinaweza
kusababisha kuendelea kwa vitendo vya ukatii dhidi ta wanawake nchini.
Viongozi
wa kijiji hicho wamekanusha kuwa hakuna uzembe uliofanyika kumkamata mtuhumiwa
huyo kwani bado inaendelea kumtafuta na kumtia hatiani.
Bi Paulina
anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospital Teule ya Seriani wilayani Arumeru
alipolazwa na hali yake bado sio nzuri.