Kwa Ufupi
“Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba alilazimika
kufanya hivyo kwani hayo yalikuwa maono ya kinabii na alifanya hivyo kwa
sababu alikuwa anatii maono aliyoonyeshwa na Mungu. Maono ambayo ni
kumpa mimba mwanamke yeyote ambaye Mungu amemchagua na kumwonyesha yeye
kwa njia ya Roho Mtakatifu bila ya kujali kama huyo ameolewa au
la,”alisema Amaraizu.
Habari Kamili
Mchungaji Timothy Ngwu (53) wa nchini Nigeria
amewapa mimba zaidi ya waumini wake 20 kwa madai ya kwamba Roho
Mtakatifu alimwabia afanye mapenzi nao.
Kiongozi huyo wa kanisa la Vineyard Trinity ambaye
hivi sasa anashikiliwa na polisi nchini humo, alifanya kitendo hicho
kwa waumini wanawake ambao wameolewa na wasichana wadogo ambao
hawajaolewa.
Akizungumza na gazeti la NAIJ na baadaye
kunukuliwa na gazeti la Jewsnews la nchini humo, Msemaji wa Kituo cha
Polisi cha Enugu ambapo Ngwu anashikilikiwa, Ebere Amaraizu alisema
wamemkamata kiongozi huyo kwa kosa la unyanyasaji wa kijinsia kwa
waumini wanawake.
“Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba alilazimika
kufanya hivyo kwani hayo yalikuwa maono ya kinabii na alifanya hivyo kwa
sababu alikuwa anatii maono aliyoonyeshwa na Mungu. Maono ambayo ni
kumpa mimba mwanamke yeyote ambaye Mungu amemchagua na kumwonyesha yeye
kwa njia ya Roho Mtakatifu bila ya kujali kama huyo ameolewa au
la,”alisema Amaraizu.
Aliongeza: “Mwanamke akijifungua atakuwa akiishi kanisani pamoja na mtoto kwa maisha yao yote.”
Mke wa mchungaji huyo ambaye baadaye alimfukuza,
Veronica Ngwu ndiye aliyeenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi
baada ya kuchoshwa na tabia hiyo hasa alipofikia hatua ya kumpa mimba
mtoto wa kaka yake.
Ndugu wa karibu wa mchungaji huyo ambaye hakupenda
jina lake litajwe alisema walimuonya kaka yao juu ya tabia hiyo, lakini
hakutaka kuwasikiliza huku akidai kuwa anatekeleza agizo la Mungu.
“Hiki kilichompata kaka yetu ni hasira kutoka kwa
Mungu kwa sababu tulimuonya lakini hakutaka kutusikiliza. Amekuwa mtemi
hapa kwetu, anawapa wanawake mimba hovyo hovyo kwa kutumia jina la Mungu
halafu ukimuonya anasema tunamuonea wivu,”alisema.
Alilalamika kuwa, Ngwu amejimilikisha sehemu ya
shamba la familia yao na kufanya kanisa lake ambalo anatumia kwa
kufanyia maovu hayo kwa jina la Mungu.
“Alimfukuza mke wake ambaye amezaa naye watoto
watatu halafu sasa hivi anafanya kazi ya kuzaa na kila mwanamke bila
kujali kama ameolewa au hajaolewa wengine ni wasichana wadogo…angalia
uwanja mzima umejaa watoto wa umri na jinsia tofauti, “alilaumu.
Ndugu huyo alisema, inashangaza kuona mtu na elimu yake anafanya vitendo kama hivyo.
MATUKIO YA KUSISIMUA ZAIDI BOFYA HAPA>>
MATUKIO YA KUSISIMUA ZAIDI BOFYA HAPA>>