Polisi
wilayani na mkoani Manyara, wanamshikilia mwalimu mmoja baada ya wenzake
kukimbia baada ya tukio.
Akizungumza
jana, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Kanali Samwel Nzoka alimtaja mwanafunzi huyo
aliyepoteza maisha kuwa ni Noel Bichima (15).
Kanali
Nzoka alisema tukio hilo lilitokea juzi asubuhi wakiwa darasani, wakati mwalimu
huyo anayeshikiliwa na polisi alipokuwa akiwafundisha. Inadaiwa mwanafunzi huyo
alichapwa viboko vinane. Haikuelezwa kama alichapwa kiganjani ama sehemu
nyingine.
Nzoka
alidai kuwa mwalimu huyo alimchapa marehemu baada ya kupata alama 40 katika
mtihani wa somo la Kiswahili kwani walipeana mkakati wa kutofeli na kwamba
mwanafunzi atakayepata chini ya alama 40 atachapwa fimbo 12.
“Mwanafunzi
huyo alifariki dunia papo hapo darasani baada ya kuanguka chini alipochapwa
viboko na walimu hao na mwili wake umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya
Kiteto ukisubiri uchunguzi,” alisema Kanali Nzoka.
“Natoa
wito kwa walimu wa shule za msingi na sekondari, kuangalia namna ya kutoa adhabu
kwa wanafunzi wanapokosea, baadhi ya watoto afya zao siyo nzuri,” alisema
Kanali Nzoka.
Diwani
wa Kata ya Matui, Athumani Kidawa alisema baadhi ya wazazi wa eneo hilo
waliopatwa na hasira baada ya kutokea tukio hilo, waliandamana hadi Kituo cha
Polisi Matui kulalamikia kitendo hicho.
Chanzo Mwananchi