Wakazi wa mitaa tofauti iliyopo kata ya Donge jijini tanga wamesema kuwa watachukua sheria mkononi dhidi ya wahalifu ambao wamekuwa wakikamatwa lakini baada ya siku kadhaa huachiwa huru kufuatia vitendo vya uvunjaji na uporaji wa mali kwa raia wema kuongezeka hatua ambayo inatishia usalama wa raia na mali zao.
Hatua hiyo inafuatia mtu mmoja
ambaye jina lake halijatambulika kupigwa mawe kisha mwili wake kuchomwa moto na
wakazi hao kwa madai kuwa yeye na wenzake watatu waliokimbia walikutwa
wakivunja duka la mfanyabiashara mmoja katika mtaa wa INDIAN OCEAN na
kufanikiwa kuiba mafuta ya kupikia aina ya sunola ambayo yalikutwa pembeni mwa
mwili wa marehemu baada ya kuchomwa.
Akielezea tukio la uporaji
lililofanywa siku moja baada ya zoezi la kumchoma moto mtu huyo anayedaiwa kuwa
ni kibaka makamu mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa donge Bwana. Michael
Chauka amesema matukio ya uporaji yanafanywa kuanzia saa moja usiku kwa kupora
simu za mikononi hasa kwa watu wa jinsia ya kike hatua ambayo imekuwa ikitishia
hali ya uaslama kwa wakazi wake.
MATUKIO YA KUSISIMUA ZAIDI BOFYA HAPA>>