JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limefanikiwa kukamata magari mawili yanayosadikiwa kutumika kubeba vitu vilivyoibwa katika Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Magari yaliyokamatwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T 989 CVN na Mitsubishi Pajero lenye namba za usajili T 386 CVV.
Aidha, limewakamata watuhumiwa watatu ambao idadi ya watuhumiwa waliokamatwa na jeshi hilo imefikia watano.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Simon Sirro alisema vitu vilivyoibwa ni kompyuta mbili aina ya Dell na runinga pamoja vifaa mbalimbali vya kompyuta ikiwemo CPU na monitor.
Sirro alisema Katibu Muhtasi wa Kamishna Mkuu wa TRA, Matrida Justus alidai kuwa aligundua kuvunjwa kwa ofisi hiyo na ya mapokezi ambapo kompyuta hizo zilikuwa ofisini kwake na nyingine ziliibwa mapokezi.
Chanzo: HabariLeo