MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Iringa imemhukumu Johnface Lyang’oka ambaye
ni mkazi wa Magozi, Pawaga wilayani Iringa kifungo cha miaka 15 jela au
kulipa faini ya Sh bilioni 1.65. Amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana
na makosa mawili yaliyomhusisha na biashara ya meno ya tembo 34.
Lyang’oka alifikishwa mahakamani hapo pamoja na mtuhumiwa mwingine katika kesi hiyo, Halfani Balobani baada ya kukamatwa Julai 30, 2015 akituhumiwa kutenda makosa hayo kati ya Julai 16 na 18, 2015.
Mahakama hiyo ilimuachia huru, Balobani aliyekuwa mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo iliyohusisha watuhumiwa wengine wanne, ambao hawajakamatwa baada ya Lyang’oka aliyekuwa mshtakiwa wa pili kukana kumfahamu mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo.
Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Andrew Scout alisema; “Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.”
Alisema Mahakama imemuona Balobani hana hatia baada ya mshtakiwa mwenza kukana kumfahamu na badala yake kuwataja watu wengine wanne ambao hawakufikishwa mahakamani hapo kwakuwa hawajakamatwa na Polisi ili waunganishwe katika kesi hiyo.
“Kwa hiyo Mahakama yangu imemtia hatiana kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa Johnface Lyang’oka na ninamhukumu kama ifuatavyo,” alisema. Alisema katika shtaka la kwanza linalomhusisha Lyang’oka na biashara ya meno ya tembo kinyume na Kifungu cha Sheria 80(1) na 84(1) ya Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009 inayokwenda sambamba na Kifungu cha 14 (d) na Kifungu cha 57 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2002 anahukumiwa: “Kwenda jela miaka 15 au faini ya Sh 1,548,000,000 baada ya kuuza meno ya tembo 32 ambayo kwa wakati huo yalikuwa na thamani ya Sh 516,000,000,” alisema hakimu huyo.
Alisema katika shtaka la pili, mtuhumiwa katika kipindi hicho hicho, alijihusisha na biashara ya meno ya tembo mawili ambayo wakati huo yalikuwa na thamani ya Sh 32,250,000 kinyume na sheria hiyo.
Scout alisema kwa mujibu wa sheria hiyo ya wanyamapori, mtuhumiwa akikutwa na hatia anatakiwa kulipa mara tatu ya thamani ya meno ya tembo kwa wakati huo, hivyo kwa makosa hayo mawili Lyang’oka anatakiwa kulipa faini ya Sh 1,644,750,000 au jela miaka 15.
MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>