Mgongo ulioathirika na Ugonjwa wa Kaswende.
Ili kuepuka na maambukizi ya Magonjwa ya ngono kijana zingatia haya yafuatayo hapa
- Usifanye Kitendo cha ngono kabisa
- Jiepushe kufanya tendo la Kujamiiana katika Umri mdogo.
- Jiepushe na ulevi na madawa ya kulevya.
- Jiepushe na vitendo vya Ubakaji.
- Jihadhari na kupiga denda na Mwenzi asiyejua hali yake ya afya.
- Jiepushe na vitendo vya kunyonya Uume au uke wa Mwenza.
- Tumia muda wako mwingi katika masomo, kazi za mikono, michezo na sanaa.
- Epuka vishawishi kama vile Zawadi na lifti za magari barabarani.
- Epuka kukaa na mpenzi wako Pekeenu hasa nyakati za usiku.
- Epuka makundi ya vijana Walevi, Wazurulaji, na Wavuta bangi au Watumiaji wa madawa ya kulevya.
- Ikiwa umeoa au kuolewa Kuwa mwaminifu kwa mwenzi wako katika tendo la kujamiiana.
KINGA DHIDI YA MAGONJWA YA NGONO
- Acha ngono kabisa katika Umri mdogo.
- Tumia kondomu ya Kike au ya Kiume kwa usahihi kwa kila tendo la Kujamiiana.