Wateja wakiwa katika meza moja wapo ya biashara wakichagua nguo za mtumba
 
Watanzania wengi wamezoea kununua nguo za mitumba kulingana na bei na wengine wanadai kuwa na ubora tofauti na zile za dukani, Lakini jambo hili linahatarisha usalama wa watumiaji wa nguo hizo.

Dar es salaam: Kaimu Mkurugenzi anayehusika na udhibiti Ubora wa TBS, Mery Meela amezungumza na chanzo chetu na kusema kuwa Nguo hizo hasa za ndani ni hatari sana kwa afya ya mtumiaji.

Watu wengi wamekuwa na kawaida ya kununua nguo za ndani ambazo tayari zimekwishakutumika na kubatizwa jina la Mtumba.

Mkurugenzi Meela amesema kuwa kuna hatari kubwa sana kwa mtu anaye tumia nguo hizo kupata maambukizi ya magonjwa ambayo anaugua yule aliyekuwa anazitumia kabla hazijaletwa Tanzania na kuitwa Mtumba. Alisema kuwa magonjwa hasa magonjwa ya ngozi ni rahisi sana kuenezwa na nguo za namna hiyo.

Hivyo watanzania wameaswa kuacha matumizi ya nguo hizo ili kuua soko la nguo za ndani za mtumba hapa nchini kwetu. Zoezi la kuzuia matumizi ya nguo hizo ni gumu sana kwasababu hakuna sheria iliyosimama kwaajili ya kuzuia biashara hiyo.

"Leo hii ukimuuliza mtu kwanini ananunua nguo za ndani za Mtumba atakwambia sababu ni bei rahisi. Lakini ukweli ni kwamba nguo mpya za ndani zinauzwa kwa bei ndogo sana kiasi cha mtu yoyote kuweza kumudu gharama, hivyo hakuna sababu ya kutumia nguo za ndani za mtumba na Kuhatarisha maisha yetu" alisema Mkurugenzi Melela.
 
Top