Katika tukio jingine, Ndaki alisema kuwa dereva wa bodaboda, Juma Said
alinusurika kuuawa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi.
Watu hao walimkodi kijana huyo kabla ya kumvamia na kumpiga kwa lengo la
kupora chombo chake cha moto, jaribio ambalo lilishindikana.
Kamanda Ndaki alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 6:00 usiku katika maeneo
ya Magomeni, mjini Tanga.
Alisema wakati wakibishana na kutishia kupigana, mmoja wa majambazi hao
alitoa sime na kumtaka aondoke ili aepuke kukatwa mikono na miguu yote.
Alitoa wito kwa madereva hao wa bodaboda kuwa na umoja na kufanya
mawasiliano katika vituo vyao, hasa anapotokea mmoja wao kukodiwa nje ya mji
wakati wa usiku.
Crdt: Mwananchi
