Wanachama wa chama cha Albino wakitembelea kisiwani ambako wanaishi walemavu wa ngozi.
Mara kwa mara Mtobi anamtazama mke wake, Sabina, ambaye ameketi kwa mkeka
kando yake akitayarisha chakula cha jioni. Watoto wake wengine wawili
wanachezea hapa karibu na pia wamejaliwa na mtoto mchanga amabye yuko chumbani
analala.
May alipokuwa na umri wa miezi mitatu, aliponea jaribio la kutekwa nyara.
" nilikuwa nimeenda ziwani kuvua samaki. walikuwa pekee yao nyumbani
wavamizi walipokuja, mke wangu alitorokea kwa dirisha na kukimbillia usalama
akiwa na May, na akawawacha watoto hawa wawili nyumabani ambao hawakuwadhuru
kabisa", Mtobi ananiarifu.
"Wavamazi hao walikuwa wakimtaka May," Sabina anaongezea,
"mume wangu alikuwa ameenda safari ya uvuvi na wavamizi hao walijua na hio
ndio sababu walikujia mtoto wangu, baada ya kutorokea kwa dirisha, bado
waliniandama huku nikipiga mayoye ya usaidizi, waliwacha kuniandama wakati tu
niliwaamsha majirani"
May ni mojawapo wa Albino sabini wanaoishi katika kisiwa hiki cha Ukerewa
ambacho ni masaa matatu tu kutoka mwanza, mji wa pili mkubwa zaidi Tanzania.
Elimu kwa jamii
Mtobi anasema "tunaiomba serikali kufanya juhudu zaidi za kuelimisha
jamii hapa, serikali ishawahi kuandaa majadiliano kuhusu Albino na kulikuwa na
mabadiliko makuwa, akini si hivyo tena"
Shirika lisilo la kiserekali chini ya mrengo wa 'The Same Sun'
linalowashughulikia jamii ya Albino hapa Ukerewa, linasema kuwa kisiwa hiki
hakina usalama kando na vile watu wangependa kuamini
Mwenye kiti wa chama cha maalbino tawi la Mwanza, (TAS) Alfred
Kapole, mzaliwa wa Ukerewe, alilazimika kutorokea mji wa Mwanza akiwa
mmoja wa albino wa kwanza kufika kortini baada ya kiognozi mmoja wa
kijiji akitaka kumuua kwa ajili ya nywele zake.
Mwaka uliopita boma lake lilivamiwa, kwa bahati nzuri alikuwa ameenda mwanza. Kulikuwa na jairibio lEngine la kumuua mwaka huu.
Kampeni kabambe
Serikali ya Tanzania imeanzisha kampeni ili kuchangisha fedha za kuelimisha jamii.
Kampeni nyingi za uhamasishaji hufanyika mijini kwani ni rahisi kufikia watu,lakini ni vijiji ndivyo vinahitaji msaada zaidi.
Ramadhan
Khalfan, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha albino Ukerewa,anasema kuwa
wanataka kufikia maeneo ya vijiji na kuzungumza na watu,lakini ni vigumu
kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha.''Hatuna uwezo ama njia za
kufikia jamii zilizoko vijijini.Aliongezea kusema,''tunategemea pakubwa
redio na televisheni,lakini hatuwezi kufika mashinani kwa sababu ya
gharama.''
Sehemu ya Serengema inapatikana kilomita 60 (maili 33.5) kutoka
Mwanza.Ili kusisitiza shida hii,umejengwa mnara katika mzunguko katikati
ya mji.
Ni sanamu ya chuma kimo cha binadamu,inayoonyesha baba
mwenye rangi akimbeba begani mto wake albino huku mama yake mwenye rangi
akitundika kofia yenye ukingo mpana kwenye kichwa cha mwana huyo
kumkinga kutokana na miale ya jua.Pia kuna majina ya watu 139 ya
waathiriwa waliouawa,kuvamiwa ama miili yao kuibiwa kutoka kwenye
makaburi. Endelea>>