Serengema ndio sehemu iliyoathirika vibaya zaidi.
Kuna
mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi pamoja na chama
cha Tanzania Albino katika kuhamasisha na pia kujenga makaazi.
Mashirika yasiyo ya kiserikali yanaamini kuwa uhamasisho na kuacha imani potovu zinaweza kusimamisha mauaji haya.
Mwakilishi wa chama cha Serengema Mashaka Benedict anasema kuwa watu
bado wanaamini kuwa sehemu za mwili wa albino zinaweza kuleta
utajiri.''Kama hiyo ndiyo hali,mbona sisi si matajiri?''anauliza.
Anadai
kuwa watu mashuhuri wanahusika katika ''biashara ya mauaji'' na ndio
maanake watu wachache sana wamekamatwa,kushitakiwa,kupatikana na hatia
ama kufungwa.''Itakuwa vipi masikini kutoa dola 10,000 kwa kipande cha
mwili?,ni wanabiashara na wanasiasa ndio wanaohusika.''
Hata hivyo
polisi wanasema kuwa wanachungunza kila moja ya visa lakini wanakosa
ushahidi wa kuthibitisha madai yanayotolewa.Kamanda wa polisi wa
Mwanza,Valentino Mlolowa anasema,''Kesi hizi ni ngumu kwa kuwa visa
hufanyika mashinani sana katika sehemu ambazo hazina stima kwa mfano,na
hiyo inafanya kuwajua wahalifu usiku kuwa vigumu.Tunachunguza kila moja
ya kesi na madai,lakini kama uonavyo,si rahisi.''
Yaweza onekana
kama kuwa tumepoteza kila kitu lakini hii haiwazuilii watu wanaoishi na
hali ya Uhalbino kama May Mosi,kutokuwa na tumaini kuwa fedha
zinazochangishwa kutoka kwenye kampeni iliyoanzishwa na serikali
zitasaidia kusikizwa zaidi kwa Albino nchini Tanzania.
Cdt: BBC