Taasisi hiyo ipo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, MNH jijini Dar es
Salaam, ambapo daktari huyo anadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu
kutoka kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa kwa madai kwamba angemhudumia mgonjwa
wao.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo,
Mkurugenzi wa MOI, Athumani Kiloloma, alisema mara ya kwanza alikamatwa Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS, akijifanya mwanafunzi wa
shahada ya uzamili katika shule ya tiba.
Dk. Kiloloma alisema alipokamatwa mara ya kwanza, walitoa matangazo katika
hospitali nzima na kutoa taarifa kwa wananchi, lakini wanashangaa tukio hilo
limejirudia tena.
Akizungumzia tukio hilo, mkurugenzi huyo alisema wanakabiliwa na tatizo
kubwa la madaktari feki, ambao wamekuwa wakiomba michango mbalimbali ya fedha.
Mtuhumiwa Dismas Macha anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka
yanayomkabili.
Awali, Dismas akizungumza na waandishi wa habari, alisema yeye si daktari
bali ni mgonjwa wa akili. Matukio ya madaktari feki yamekuwa yakiripotiwa
katika hospitali mbalimbali nchini Tanzania katika siku za karibuni, ambapo
inadaiwa madaktari hao kazi kubwa ni kuwatapeli wagonjwa na ndugu wa wagonjwa.
Crdt: BBC