
Akitoa hukumu hiyo jana Kiongozi wa jopo la Mahakimu
watatu wanaoisikiliza kesi hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu, Edson Mkasimongwa
alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa
mashtaka na utetezi wa washtakiwa hao anaona upande wa mashtaka umeshindwa
kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka.
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Johnson
Lukaza na mdogo wake Mwesigwa Lukaza baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi
ya wizi wa wa Sh 6.3 bilioni za akaunti ya madeni ya Nje (EPA) iliyopo
Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Akitoa hukumu hiyo jana Kiongozi wa jopo la Mahakimu
watatu wanaoisikiliza kesi hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu, Edson Mkasimongwa
alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa
mashtaka na utetezi wa washtakiwa hao anaona upande wa mashtaka umeshindwa
kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka.
Mashtaka matano yaliyokuwa yakiwakabili hao ni pamoja kula njama, kughushi,
kuwasilisha hati za uongo za makubaliano ya kuhamisha deni kati ya
kampuni yao ya Kernel Ltd na kampuni Marubeni ya nchini Japan na
kujipatia kiasi hicho cha fedha cha Sh 6.3 bilioni kwa njia ya udanganyifu.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mkasimongwa amesema wamewaachia huru
washtakiwa hao katika makosa hayo yote kwa sababu ushahidi wa upande wa
mashtaka haukujitosheleza kwa kuwa ulishindwa kuthibitisha kama ni kweli
Novemba 2,2003 washtakiwa hao walighushi hati ya makubaliano ya
kuhamisha deni la Sh 6.3 bilioni baina ya kampuni ya Kernel Ltd na
Marubeni ya nchini Japan ilikuwa ni ya kughushi.
Jaji Mkasimongwa anasema ushahidi unaonesha kampuni hiyo ya Marubeni ya
nchini Japan ilikubali kupokea kiasi hicho cha fedha na kwamba
washtakiwa wao walipata asilimia tu ya 20 ya fedha hizo na upande
wamashtaka hakuwahi kulibishia hilo.
Katika kesi hiyo, Johnson Lukaza ambaye ni Mwenyekiti wa makampuni ya
Proin na ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) pamoja na mdogo
wake Mwesiga walikuwa wanatetewa na Wakili Alex Mgongolwa aliyekuwa
akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi.
Baada ya hukumu hiyo kutolewa ndugu wa washtakiwa hao waliaza kulia
mahakamani hapo pamoja na mshtakiwa Mwesiga wakiwa hawa amini kilichotokea huku
wakisema asante Yesu, asante Yesu.
Cedt: Mwananchi.