
Mashuhuda wa tukio hili walisema kijana huyo na wenzake waliiba pikipiki mbali na hapo Mwembechai ila katika purukushani na wamiliki wa chombo kile, kijana yule alijikuta akianguka kutoka kwenye pikipiki





Gari la Polisi likiwa eneo la tukio



KIJANA ambaye jina lake haikufahamika
mara moja, amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kwa tuhuma za wizi wa
pikipiki jijini Dar.Tukio hilo la kusisimua limetokea asubuhi ya leo
Magomeni-Mwembechai, ambapo lilisababisha foleni ndefu ya magari
wakati kijana huyo akiadhibiwa na wananchi.
Mashuhuda wa tukio hili walisema
kijana huyo na wenzake waliiba pikipiki mbali na hapo Mwembechai ila katika purukushani
na wamiliki wa chombo kile, kijana yule alijikuta akianguka kutoka kwenye
pikipiki eneo lile na kuzingirwa na waendesha pikipiki wa pale wanaojulikana
kama ‘bodaboda’ walioanza kumshushia kipigo baada ya mmiliki wa pikipiki husika
aliyekuwa akiwafukuza kusema kijana huyo alikuwa na wenzake waliokimbia na
chombo hicho.
Pamoja na kipigo alichopewa,
wananchi waliamua kumvisha tairi shingoni wakiwa tayari kumchoma moto ambapo
dakika chache tu baadaye askari walifika na kumwokoa.
Kijana huyo aliyekuwa bado hai, aliokolewa na askari wa doria waliomchukua pamoja na mtu aliyejitaja kama mmiliki wa pikipiki iliyoibiwa.
Crdt: BBC
Kijana huyo aliyekuwa bado hai, aliokolewa na askari wa doria waliomchukua pamoja na mtu aliyejitaja kama mmiliki wa pikipiki iliyoibiwa.
Crdt: BBC