Baada ya vuta nikuvute kati
ya Askari na wana ndugu hao ndipo wana ndugu walipoamua kumshambulia askari
huyo kwa kumpiga na panga Kivuyo kwenye miguu na mikono kisha kumpiga kwa nondo
kichwani.
Mtu mmoja mkoani Tanga wilayani
Kilindi katika kijiji cha Kwamazandu, aliefahamika kwa jina la Godfrey Kivuyo (34)
askari wa jeshi la Mgambo, amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa na mapanga kwenye
miguu, mikono na kupigwa nondo kichwani.
Bwana Kivuyo amekumbana na
kipigo hicho alipokuwa amekwenda kumkamata Mtuhumiwa Omari Bakari (34) ambaye
alikuwa akikabiliwa na kesi ya mgogoro wa ardhi. Kwa mujibu wa chanzo chetu
kimeeleza kuwa Bwana Kivuyo alipofika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo alikutana na
ndugu zake ambao waligoma kukamatwa kwa ndugu yao Omary.
Baada ya vuta nikuvute kati
ya Askari na wana ndugu hao ndipo wana ndugu walipoamua kumshambulia askari
huyo kwa kumpiga na panga Kivuyo kwenye miguu na mikono kisha kumpiga kwa nondo
kichwani.
Kaimu kamanda wa Polisi mkoa
wa Tanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Juzi saa 10:30 Jioni katika
kijiji cha Kwamazandu. Amesema kuwa, Watuhumiwa wote sita wanashikiriwa na
jeshi la polisi kwaajili ya kujibu shitaka hilo.
Watu ambao wanashikiliwa
kuhusiana na tukio hilo ni pamoja na Omari Bakari (38), Abdala Bakari (35),
Haji Mohamedi (21), Halima juma (28), Mwajabu Salim (35), na Mohamed Seleman
(34), wote hao ni wenyeji wa Kwamazandu wilayani Kilindi.