Songea. Mkazi wa Kijiji cha Majimaji, Kata ya Chalinze,
wilayani Tunduru (jina linahifadhiwa), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za
kumkata sehemu za siri mume wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alisema
kuwa tukio hilo limetokea jana saa tisa usiku baada ya kutokea mzozo kati yao.
Kamanda Msikhela alisema mwanaume huyo (jina linahifadhiwa),
amejeruhiwa sehemu za siri na kwamba chanzo cha yote hayo ni wivu wa mapenzi.
Alisema majeruhi huyo kwa sasa amelazwa Hospitali ya Wilaya
ya Tunduru na hali yake inaendelea vizuri.
“Tunamhoji mtuhumiwa ili kujua sababu, tukikamilisha
uchunguzi tutamfikisha mahakamani kujibu mashtaka,” alisema Kamanda Msikhela.