Watu wenye silaha wameshambulia hoteli moja ya kitalii iliyoko kwenye pwani ya Tunisia na kuwauwa watu 37.
Maafisa
wa serikali ya Tunisia wamesema kuwa mmoja wa washambuliaji hao aliuawa kwa
kupigwa risasi na maafisa wa ulinzi na kuwa waliosalia bado wanasakwa na
polisi.
Shambulio
hilo lilitokea katika mji wa Sousse, ambao huwavutia maelfu ya watalii kutoka
bara Ulaya na Afrika ya Kaskazini.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa
mmoja wa magaidi hao ameuawa
Hili
lilikuwa shambulizi la pili dhidi ya hoteli ya watalii nchini Tunisia katika
kipindi cha miezi michache iliyopita.
Inaaminika
kuwa washambuliaji hao waliwavamia watalii ufukweni.
Mnamo
mwezi Machi mwaka huu, wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki
waliwauawa zaidi ya watu 26 katika makavazi ya Bardo, iliyoko katika mji mkuu
wa nchi hiyo Tunis.
Makavazi
hayo ya Bardo hilo lilikuwa maarufu sana kwa watalii.
October
mwaka wa 2013, mlipuaji wa kujitoa, alijilipua nje ya nyumba moja mjini Sousse,
baada ya maafisa wa polisi kutibua jaribio lake la kutaka kuingia ndani na
kuishambulia.